Jumapili 18 Oktoba 2026 - 06:42
Kung’ara vijana wa Iran katika medani za kimataifa ni chanzo cha matumaini ya mustakabali mwema

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, katika ujumbe wake, aliipongeza timu ya taifa ya Iran ya mieleka, yenye wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23, kwa kutwaa ubingwa katika Mashindano ya Dunia yaliyofanyika nchini Marekani. Aidha, alieleza kuwa kung’ara kwa vijana hao ni chanzo cha matumaini ya kuwa na mustakabali mzuri na wenye mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husayni Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alitoa ujumbe wa kuipongeza timu ya taifa ya Iran ya mieleka, yenye wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23, kwa kutwaa ubingwa katika Mashindano ya Dunia.

Maandishi kamili ya ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Ninaupongeza ubingwa uliotwaiwa na timu ya taifa ya Iran ya mieleka, yenye wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23, katika Mashindano ya Kimataifa ya Vijana wa Chini ya Miaka 23 ya Dunia yaliyofanyika nchini Marekani. Pongezi hizi ninazitoa kwa mabingwa hawa walioiletea nchi heshima na fahari, makocha wao wanaofanya juhudi kubwa, pamoja na wananchi wote wa Iran.

Kung’ara kwa vijana wa nchi yetu, kupeperushwa kwa fahari bendera ya Iran kunakoibua shauku na furaha, pamoja na kusikika wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika medani mbalimbali, ni mwangaza wa matumaini ya wananchi kwa vijana wao katika safari ya kufikia mustakabali wenye mafanikio makubwa na utukufu.

Dua zangu za heri ziambatane na safari ya vijana wote wa Iran yenye fahari.

Sayyid Mujtaba Husayni Khamenei

25 Mehr 1405 (17 Oktoba 2026)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha